Jumatatu 10 Novemba 2025 - 21:13
Athari za kihistoria za Ghaza bado zinahifadhiwa katika Makumbusho ya Geneva

Hawza/ Kutokana na uharibifu, mauaji ya kimbari na jitihada nyingi zilizofanywa na utawala katili wa Kizayuni katika kuangamiza athari za kihistoria za ardhi ya Gaza na Palestina, serikali ya Uswisi imesaini makubaliano ya ushirikiano na serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina kwa ajili ya kulinda athari hizo. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Uswisi imejitolea kuyahifadhi baadhi ya mabaki ya kale hadi pale eneo hilo litakapokuwa salama.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, vitu 44 vya kihistoria na vya kale vilivyogunduliwa Ghaza vinahifadhiwa katika Makumbusho ya Geneva, Uswisi. Miongoni mwa vitu hivyo ni mitungi ya udongo, sanamu, vyungu na taa za mafuta. Vitu hivyo vinaoneshwa katika sehemu maalumu ya makumbusho iitwayo Urithi Ulio Hatarini.

Beatrice Blandin, msimamizi wa sehemu hiyo katika makumbusho katika mahojiano alisema kwamba: “Vtu hivi ni sehemu ya historia na roho ya Ghaza, na vinaakisi historia halisi ya watu waliokuwa wakiishi huko tangia zamani.” Aliongeza kuwa mkusanyo wa Ghaza una jumla ya vipande 530 vinavyohifadhiwa katika masanduku na ghala salama huko Geneva, na kutokana na uharibifu na uhalifu wa utawala wa Kizayuni huko Ghaza, kwa sasa hakuna uwezekano wa kurejeshwa Ghaza.

Mmoja wa wajumbe wa Baraza la Jiji la Geneva alisisitiza umuhimu wa kulinda na kutunza athari hizo, akisema kuwa “vikundi vyenye fikra mgando daima huwa na azma ya kuharibu urithi wa kihistoria na wa ustaarabu.”

Chanzo: Al-Monitor.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha